
Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ,
alie fanya tarjuma hii ni Mzalendo wa Zanzibar,
aliezaliwa 13 January 1919, akapata mafunzo ya dini kwa baba yake Sheikh Muhsin bin Ali na kwa wanazuoni wengineo wa Afrika ya Mashariki.
Pia Sheikh Ali amesoma ilimu ya zaraa katika Chuo Kikuu cha Makerere (Makerere University) huko Uganda.
Alianza maisha yake kwa kufanya kazi ya zaraa na uwalimu. Katika 1947 aliacha kazi ya serikali, ili ashughulikie jihadi ya nchi yake na Umma wake.
Alikuwa Muhariri Mkuu wa gazeti la "Mwongozi" kwa muda wa miaka kumi na tano. (read more)
